Tuesday, May 31, 2016

MAALIM SIEF KIKAANGONI POLISI


Baada ya Jeshi la Polisi Zanzibar kuahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, hatimaye hatua hiyo sasa imeelekea kutekelezwa.


Taarifa rasmi ya jeshi hilo visiwani Zanzibar, imemtaka Maalim Seif afike katika Ofisi za Makao Makuu ya Polisi, Ziwani mjini hapa leo saa 4.00 asubuhi.

Friday, April 22, 2016

MBUNGE WA CHADEMA AMVAA MAGUFULI ALIPE KODI





Katika mjadala wa jana bungeni, mbunge wa CHADEMA viti maalum kutoka mkoa wa Geita, Upendo Peneza amlipua Rais Magufuli ya kwamba anapaswa kuonyesha mfano katika kulipa kodi kutoka kwenye mshahara wake ambao kwa sasa haukatwi kodi..

Hali hiyo ilizua taharuki ambapo waziri wa ofisi ya Rais, TAMISEMI Simbachawene aliinuka na kuomba kutoa taarifa. Katika kutoa kwake taarifa waziri alisema mshahara wa Rais haujadiliwi popote pale, ikiwa ni sharti ndani ya katiba ibara ya 43.

Mbunge Peneza katika kukataa taarifa hiyo alisema hoja yake ya msingi ni kutaka Rais aonyeshe kuongoza kwa mfano kwa kulipa kodi kama anavyosisitiza wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi.

Tuesday, March 22, 2016

UCHAGUZI WA MEYA KUFANYIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru uchaguzi wa meya na naibu meya wa Jiji la Dar es Salaam, kufanyika leo kama ilivyopangwa.

Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema alitoa uamuzi huo jana akijibu maombi yaliyokuwa yamewasilishwa na walalamikaji, Suzan Massawe na Saad Mohammed Kimji kupitia wakili wao,