Msanii wa Bongo Fleva Rajabu Abdulkhali ‘Harmonizer’.
Andrew Carlos
UKIZUNGUMZIA
miongoni mwa vichwa vya Bongo Fleva vinavyokuja kwa kasi kwa sasa ni
wazi utamzungumzia msanii, Rajabu Abdulkhali ‘Harmonizer’ ama wengi
wanamfahamu kama ‘mdogo’ wa Diamond kutokana nakufanana kwao sura na
muonekano.
Harmonizer amekuja kasi kunako muziki wa Bongo Fleva ambapo ndani ya wimbo mmoja alioutoa mwanzoni mwa Agosti wa Aiyola umemfanya kuwa katika ramani ya kimataifa ya muziki huu wa Bongo Fleva.
Ngoma
hiyo tangu alipoitoa amepata sapoti kubwa kutoka kwa mastaa wa Afrika
kama vile KCEE, Yemi Alade, Victoria Kimani (wote Nigeria), Mafikizolo,
Donalds (Afrika Kusini) pamoja na Juliet Ibrahim (Ghana) ambapo wote kwa
nyakati tofauti wamekuwa wakitumia mitandao yao ya kijamii kuupaisha
kwa kuachia kava na hata vipande vya wimbo huo.
Harmonizer
ambaye yupo chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) amekuwa msanii
wa kwanza kutoka ndani ya lebo hiyo inayosimamiwa na Nasibu Abdul
‘Diamon Platnumz.’
Katika makala haya, Harmonizer anafunguka zaidi;
Vikwazo vipi umepitia katika muziki?
Kikubwa
nakumbuka ilikuwa mwaka 2011 niliwahi kudhulumiwa shilingi 30,000
katika studio kubwa tu hapa Bongo (jina kapuni) na ilifika kipindi
nikataka kukata tamaa kabisa ya kuendelea na muziki.
Shoo gani hutaisahau katika maisha yako ya muziki?
Mwaka
jana kulifanyika Tamasha la Serengeti Fiesta kwenye mwezi wa 10 pande
za Mtwara. Nikapewa mchongo kuwa kule ninaweza kuonana na wasanii
wakubwa.
Nikafunga
safari na kufikia katika hoteli moja, lakini kesho yake nikiwa njiani
naelekea kwenye shoo usiku, vibaka wakanivamia na kunikwapua pesa, simu,
tisheti na viatu ikabidi nirudi hotelini niuze vitu vyangu kwa ajili ya
kupata nauli ya kurudi Dar.
Ulikutana vipi na Diamond?
Nilipotoka Mtwara kwenye Fiesta na kurudi Dar, nilikutana na DJ Milazo akanipatia namba ya Diamond.
Nikakaa
na namba hiyo ya simu kwa takribani miezi miwili nikijiuliza nitaanzaje
kumpigia simu na kujieleza akanielewa. Siku moja nikajipa moyo wa
kijasiri baada ya kuliona tangazo kwenye gazeti la shoo yake
iliyofanyika Sikukuu ya Chrismas akiwa na msanii wa Taarab, Mzee Yusuf
ambayo ilikuwa ikifanyika Dar Live ikijukana kama Usiku wa Wafalme.
Tangazo hilo likanifanya nimtumie meseji kwa kuandika;
Oy Mondi Bin Laden!
Akanijibu;
Oy!
Kwa
kweli nilijisikia faraja kweli hata marafiki zangu nilikuwa nawaonesha
meseji ile, nikamtumia tena meseji nyingine kuwa mimi naitwa Harmonizer
nafanya muziki, nilikuwa naomba nije kutambulisha wimbo wangu katika
shoo yako ya Dar Live.
Alinijibu
kiustaraabu kuwa wasiliana na huyu mtu nitakuombea kwa sababu shoo siyo
ya kwangu. Akanitumia namba ya kaka yake anaitwa Ricardo nikawasaliana
naye na kuniita Dar Live.
Nikamuomba
jamaa mmoja anishuti video na kesho yake asubuhi nikamtumia kipande cha
video Diamond, akaniuliza nipo katika menejimenti yoyote nikamwambia
hapana akaniuliza nyimbo nilizozifanya nikamtumia.
Akanipa
jibu moja tu kuwa ameenda India kumuuguza mama yake kwa hiyo akirudi
atanicheki. Akarudi na kuniita kwenye ofisi zake Sinza-Mori na kuniweka
katika lebo yake na kufanikiwa kutoka na Wimbo wa Aiyola.
Mipango ya video na ngoma nyingine?
Kwa
sasa hivi siwezi kusema sana kwa kuwa nipo kwenye menejimeti nawaachia
wao japokuwa kuna kolabo nyingi za nje ya Afrika ambazo wamekubali kazi
yangu na kutaka wanishirikishe kwenye kazi zao. Mashabiki wategemee
video ya ngoma hii itakayokuwa ya kimataifa kwani tutaitengeneza nje ya
nchi
No comments:
Post a Comment