DAR ES SALAAM.Sospeter Muhongo,waziri wa nishati na madini
Serikali imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuacha mara moja tabia ya kukata umeme bila sababu ya msingi.
Agizo hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati
na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani
walipofanya ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Wizara
hiyo.
Mara tu baada ya kuapishwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walifanya ziara hiyo
ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) na kuzungumza na Menejimenti ya Shirika hilo.
Profesa Muhongo alisema wananchi wamechoshwa na tabia ya shirika hilo
ya kukatakata umeme bila kuwepo na sababu ya msingi ya kufanya hivyo.
Haiwezekani kila mwaka matatizo ni yaleyale na nyie bado mpo ofisini,
hili halikubaliki na