Monday, April 27, 2015

ARSENAL, CHELSEA NGUVU SAWA


Santi Cazorla akipiga mpira uliomgonga mkononi beki wa Chelsea Gary Cahill wakati wa mechi ya leo.
Oscar wa Chelsea akikwaana na kipa wa Arsenal David Ospina wakati wa mtanange wa leo.
Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas akizawadiwa kadi ya njano baada ya kujirusha akitafuta penalti.
ARSENAL na Chelsea leo zimeshindwa kutambiana katika mechi yao ya Ligi Kuu ya England iliyopigwa kwenye Uwanja wa Emirates jijini London. Mpaka mwisho wa dakika 90, Arsenal 0-0 Chelsea.
Kwa matokeo ya leo Chelsea wamefikisha pointi 77 wakiwa nafasi ya kwanza huku Arsenal wakiwa na pointi 67 katika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City.
VIKOSI:
Arsenal (4-2-3-1): Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin (Welbeck 75), Cazorla, Ramsey, Ozil, Sanchez, Giroud (Walcott 82)
Waliokuwa benchi: Szczesny, Debuchy, Gibbs, Wilshere, Flamini
Chelsea (4-2-3-1): Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian (Cuadrado 90), Oscar (Drogba 46), Hazard, Fabregas (Zouma 90)
Waliokuwa benchi: Cech, Luis, Mikel, Loftus-Cheek

Saturday, April 25, 2015

BALAAAAA TENA, ANGALIA HII

Tetemeko kubwa la ardhi laikumba Nepal

 
Majengo yaliyoharibiwa Nepal
Tetemeko kubwa la ardhi limekumba eneo lililo magharibi mwa Nepal.
Shirika la utafiti la Marekani lilisema kuwa tetemeko hilo la vipimo vya 7.5 lilikumba aneo liilo umbali wa kilomita nane mashariki mwa Pokhara, magharini mwa mji mkuu Kathmandu.
Kuna ripoti za uharibifu ya majengo. Idadi ya watu waliokufa au kujeruhiwa haijulikani. Mitetemeko midogo ilisikika pia umbali wa hadi mji wa New Delhi na miji mingine kusini mwa India.

SHEREHE ZA MIAKA 100 ZAFANYIKA

Sherehe za miaka 100 zafanyika Gallipoli

Sanamu za makumbusho Gallipoli
Sherehe zimefanyika eneo la Gallipoli nchini Uturuki kuadhimisha miaka mia moja tangu uvamizi wa kijeshi uliofanywa eno hilo na wanajeshi wa muungano wakati wa vita vya kwanza vya dunia.
Zaidi ya watu 100,00 waliuwa kwenye uvamizi huo ulioendeshwa dhidi ya ufalme wa Ottoman.
Wageni kutoka nchi zote zilizopigana walihudhuria sherehe hizo wakiwemo viongozi kutoka Uturuki , Australia na New Zealnd, ambazo zote zilipoteza watu wengi.
Sherehe pia zilifanyika mapema nchini New Zealand na pia mjini Sydney. Zaidi ya wanajeshi 10,000 wa Australia na New Zealand waliuawa kwenye vita hivyo vilivyofeli.