Tuesday, July 28, 2015

HALI NGUMU YA MAISHA HADI MBUNGE KUONYESHA NGUO ZA NDANI


mbunge zimbabwe
Unamkumbuka yule Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola aliyeingia Bungeni na bidhaa za kichina huku akiilaumu Serikali kushindwa kutumia rasilimali zake na kutegemea bidhaa za nje?.
Hii nyingine imetokea Zimbabwe na kuzua kizaazaa baada ya Mbunge wa upinzani Priscilla Misihairabwi kutinga Bungeni akiwa na nguo za ndani za wanawake huku akisisitiza hatma ya raia wake maskini kutokuwa na uwezo wa kununua nguo hizo.
Katika kikao chicho cha bunge kilichokuwa kikirushwa live na Televisheni ya Taifa, mbunge huyo wa Chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change ‘MDC‘ alitoa mfuko wa plastiki uliokuwa na nguo hizo.
BUNGE
Bunge la Zimbabwe
Baada ya kutoa akamuuliza Waziri wa Fedha na sera za serikali kuhusiana na uingizwaji wa nguo hizo za mtumba  ambazo bei yake ni ndogo na husababisha madhara kwa akina mama.
Akijibu swali hilo Waziri wa Fedha Patrick Chinamasa alimtania Mbunge huyo kutokana na uamuzi wake wa kubeba nguo za ndani za akina mama lakini akasema Wizara yake  inachunguza suala hilo.
Kufuatia kitendo hicho Mbuge huyo alitolewa ndani ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa chama tawala cha ZANU PF  kwa madai ya kutumia matamshi ya kibaguzi.
Uchumi wa Zimbabwe umedorora miaka ya hivi karibuni hali iliyosababisha viwango vya umaskini kuongezeka kutokana na kuwepo idadi kubwa ya watu wasio na ajira.

Tuesday, July 21, 2015

KIVUMBI TENA, KLABU BINGWA BARANI ULAYA (UEFA)


 

Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya inaendelea tena hii leo kwa timu zile zinacheza round ya kwanza ambapo Dila Gori ya Geogia itakuwa na kibarua kigumu itakapoumana vikali na Partizan Belgrade ya Serbia.
Huku FC Pyunik ya Armenia ikikutana uso kwa uso na Molde ya Norway.
Milsami ya Boldova itapimana nguvu na Ludo Bulgaria.
Mechi nyingine za Klabu Bingwa barani Ulaya hapa chini

Dila Gori v Partizan Belgrade 13:30

FC Pyunik v Molde 15:00

Milsami Orhei v Ludo Razgd 16:00

HJK Helsinki v FK Ventspils 17:00

Maccabi Tel Aviv v Hibernians FC 18:30

Lincoln Red Imps v FC Midtjylland 19:00

Vardar v Apoel Nic 19:00

Zalgiris v Malmö FF 19:10

Crusaders FC v Skenderbeu Korce 19:45

Saturday, July 18, 2015

DUKA LILILOSHAMBULIWA KENYA LAFUNGULIWA LEO



                                                      Duka la Westgate kufunguliwa leo


Duka la westagate lililo mji mkuu wa Kenya Nairobi linafungua milango yake hii leo kwa umma karibu miaka miwili tangu lishambuliwe na wanamgambo wa al shabab.
Watu 67 waliuawa wakati wa makabiliano ya siku nne wakati wanamgambo hao walipowafyatulia risasi wateja.
Duka hilo linafunguliwa wiki moja baada ya rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara nchini kenya hatua inayoonekana kama ishara ya imani kwa usalama wa nchini Kenya.
Al Shabab wameendesha mashambulizi mengine mabaya nchini Kenya tangu litokee shambulizi la Westgate likiwemo la chuo kikuu cha Garissa ambapo watu 150 waliuawa