Mchawi wa Barcelona, Lionel Messi ameonekana mtulivu kwenye mazoezi ya jana akijiandaa na mechi ya UEFA Super Cup.
Siku
chache zilizopita, Messi alicheza dhidi ya AS Roma katika mechi ya
kirafiki dhidi ya AS Roma ya Italia, lakini ndani ya uwanja kulikuwa na
cheche za aina yake.
Messi alimpiga kichwa na kumkaba koo beki wa Roma, Mapou Yanga-M'Biwa, Barcelona ikishinda 3-0 Camp Nou.
Muargentina huyo hakuoneshwa kadi nyekundu kwa kufanya tukio hilo.
Mwishoni mwa juma lililopita Mayweather (kushoto) alitunukiwa tuzo ya Nevada Boxing Hall of Fame
Wakati
huu akijiandaa kupanda ulingoni mwezi septemba mwaka huu dhidi ya Andre
Berto, Floyd Mayweather aliomba ataje mabondia watano wakubwa zaidi
kuwahi kutokea duniani.
Mayweather
aliwashangaza watangazaji wa TV ya ESPN mjini Los Angeles baada ya
kujitangaza mwenyewe kuwa ndiye bondia bora zaidi wa wakati wote.
Mr Money alijiita ni mtu wa ajabu zaidi kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa masumbwi.
Mayweather
alisema: "Nimewapiga mabingwa zaidi wa dunia kuliko bondia yeyote ndani
ya muda mfupi. Nimewapiga wengi zaidi na nimepigwa kidogo sana".
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (pichani) amezungumzia kukosekana
kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa katika vikao vya chama
hicho vinavyoendelea jijini, akisema: “Nitazungumzia suala hilo muda
muafaka ukifika.”
Mbowe alisema hayo jana katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach kilipokuwa
Beki wa kulia wa Manchester United, Rafael da Silva
Klabu
ya Lyon ya Ufaransa imemsajili beki wa kulia wa Manchester United
Rafael da Silva kwa mkataba wa miaka minne na kwa kitita ambacho
hakikutajwa.
Rafael mwenye miaka 25 alijiunga na Manchester United akiwa na pacha wake Fabio kutoka Fluminense mwaka 2008.
Katika msimu uliopita beki huyu alianza katika michezo sita tu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mara kwa mara.
Kupitia mtandao wake wa twitter Rafael aliandika "nataka kuwashukuru mashabiki kwa mapenzi kwa miaka minane niliyokuepo hapo''
Rafael amecheza jumla ya michezo 170 na akifunga mabao 5 pacha wake Fabio alijiunga na Cardiff City katika msimu wa 2014.