Wednesday, September 30, 2015

AENDELEA NA ZIARA YAKE DODOMA:MAGUFULI

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE,KESHO KUUNGURUMA LIVE UWANJA WA JAMHURI MKOANI DODOMA

 Pichani kati ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiwa sambamba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde kwa pamoja wakiwapungia wananchi wa jimbo la Mtera (hawapo pichani),ndani ya mji wa Mvumi wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
 Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  Wakazi wa jimbo la Mtera huku akiwamwagia sera zake za kuomba kura za kuwania nafasi ya Urais katika awamu ya kipindi cha tano,mapema jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibakwe,Wilayani Mpwapwa,Ndugu Dkt.Simba Chawene akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa kijiji cha  Chipogolo (hawapo pichani),wakati akitokea Iringa vijijini akielekea mkoani Dodoma kuanza kampeni zake mkoani humo,kulia kwake ni Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwatazama wananchi waliokuwa wakimuuunga mkono kuwa watampa kura za ndio 
 Dkt Magufuli akiwapungia Wananchi wa kijiji cha Chipogolo Wilayani Mpwapwa,mara baada ya kuwahutubia mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni,shoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Alhaji Adam Kimbisa.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Kada mkongwe wa chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.John Samuel Malecela akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni.
Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni  uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo mapema leo asubuhi mkoani Iringa wakati wa kumnadi Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli
  wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo mapema leo asubuhi mkoani Iringa wakati wa kumnadi Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli 
 Wanannchi wakifuatilia mkutano wa Dkt Magufuli katika kijiji cha Pawaga na Idodi mapema leo asubuhi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni akimalizia kiporo cha baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Iringa aliyoanza kampeni zake hapo juzi mkoani humo,ambapo leo amewasili mkoani Dodoma na kuanza kampeni zake wilayani Mpwapwa katika jimbo la Kibakwe na baadae jimbo la Mtera.

Monday, September 28, 2015

CHEKI HII YA MAGUFULI

Posted by Williammalecela.com on Monday, September 28, 2015
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaiambisha wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Mafinga mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
 Mmoj wa Waangalizi wa Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,akifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli mjini Makambako jioni ya leo Septemba 27 mkoani Iringa
????????????????????????????????????

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Ndugu Mahmoud Mgimwa akipiga push up mbele ya wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli  ambaye anashuhudia tukio hilo katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vyaWambi 

Saturday, September 26, 2015

DOGO’ WA KING WA POP BONGO DIAMOND ALIYEWATEKA WANAIJERIA


Msanii wa Bongo Fleva Rajabu Abdulkhali ‘Harmonizer’.
Andrew Carlos
UKIZUNGUMZIA miongoni mwa vichwa vya Bongo Fleva vinavyokuja kwa kasi kwa sasa ni wazi utamzungumzia msanii, Rajabu Abdulkhali ‘Harmonizer’ ama wengi wanamfahamu kama ‘mdogo’ wa Diamond kutokana nakufanana kwao sura na muonekano.
Harmonizer amekuja kasi kunako muziki wa Bongo Fleva ambapo ndani ya wimbo mmoja alioutoa mwanzoni mwa Agosti wa Aiyola umemfanya kuwa katika ramani ya kimataifa ya muziki huu wa Bongo Fleva.
Ngoma hiyo tangu alipoitoa amepata sapoti kubwa kutoka kwa mastaa wa Afrika kama vile KCEE, Yemi Alade, Victoria Kimani (wote Nigeria), Mafikizolo, Donalds (Afrika Kusini) pamoja na Juliet Ibrahim (Ghana) ambapo wote kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitumia mitandao yao ya kijamii kuupaisha kwa kuachia kava na hata vipande vya wimbo huo.

Friday, September 25, 2015

UJUMBE WA LEO KATIKA VIBONZO



MGOMO WA WAALIMU KUSITISHWA NA MAHAKAMA

zako
Mahakama nchini Kenya imesimamisha mgomo wa walimu uliodumu kwa wiki nne na kuwaagiza walimu kurudi kazini mara moja.
Jaji Nelson Abuodha wa mahakama ya kiviwanda na masuala ya wafanyakazi amesimamisha mgomo huo kwa miezi mitatu na kuwataka walimu na serikali kuunda kamati ya kutafuta suluhu katika muda wa mwezi mmoja.
Aidha, ameiagiza Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) kutowaadhibu walimu na kuwalipa mishahara yao kikamilifu, pamoja na marupurupu. Tume hiyo ilikuwa awali imetishia kutowalipa walimu “kwa siku ambazo wamesusia kazi”.
Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo katika kesi iliyokuwa imewasilishwa na TSC kutaka mgomo wa walimu uliosababisha kufungwa kwa shule zote za umma kutangazwa kuwa “usiolindwa kisheria”.
Jaji Abuodha alisema mahakama inaweza tu kuamua kuhusu uhalali wa mgomo na akasema pia kuwa wafanyakazi wana haki kugoma.
Maafisa wa Chama cha Kitaifa cha Walimu (KNUT), moja ya vyama vilivyokuwa vimeitisha mgomo huo, hawajazungumza na wanahabari baada ya uamuzi huo lakini wameahidi kutoa taarifa.
Walimu waligoma wakitaka kulipwa nyongeza ya mishahara ya asilimia 50 hadi 60 ambayo mahakama ilikuwa imeagiza walipwe.
Wiki iliyopita, Rais Uhuru Kenyatta alisema serikali haiwezi kulipa nyongeza hiyo.
Mgomo huo ulikuwa umetishia kuvuruga mitihani ya kitaifa inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Baraza la Kitaifa la Mitihani Kenya (KNEC) kuna watahiniwa 937,467 wanaojiandaa kufanya mtihani wa darasa la nane KCPE utakaoanza Novemba 10 na kumalizika Novemba 12.
Watahiniwa wanaojiandaa kufanya mtihani wa kidato cha nne KCSE utakaoanza rasmi Oktoba 12 ni 525,802.

WAZIRI CELINA KOMBANI AFARIKI DUNIA


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani amefariki dunia nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu
Taarifa tulizozipata usiku huu zimesema kuwa Waziri Kombani ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Ulanga Mashariki kupitia chama cha Mapinduzi, mwili wake utawasili nchini Jumamosi ya Septemba 26 mwaka huu
Mtandao huu unatoa pole kwa familia ya marehemu na taifa kwa ujumla kwa msiba huu.
VIA:http:www.mpekuzihuru.com

Wednesday, September 23, 2015

MBUNGE AMNYONYESHA MTOTO WAKE BUNGENI.


Argentinian MP Victoria Donda Perez has won global praise after being photographed breastfeeding her 8-month-old daughter while attending a parliamentary
session at the Congressional Palace in the capital Buenos Aires.

Tuesday, September 22, 2015

KAJITOA MBIO ZA URAIS

Walker ajitoa mbio za urais Marekani

scott Walker
Scott Walker, ambaye ni miongoni wagombea waliokuwa wakiwania kuteuliwa kugombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican amejiondoa kutoka kwa kinyanganyiro hicho.
Bwana Walker ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Winscosin amesema amejitoa kutoka kampeini hizo ili kutoa nafasi kwa uteuzi wa mgombea muafaka atakayekabiliana na Donulkd Trump.
Mgombea huyo, ambaye alikuwa akiungwa mkono kwa wingi na wafuasi wa mrengo wa kulia, lakini hata hivyo katika kura ya maoni kiwango chake kilishuka baada ya kufanya vibaya katika midahalo. Scott Walker, mmojawapo wa wagombea watarajiwa wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican amejiondoa kutoka kwa kinyanganyiro hicho.