Sunday, December 27, 2015

WAZIRI MKUU KUNUSURIKA AJALI YA NDEGE LEO 27/12/2015


Waziri mkuu wa Benin, Lionel Zinsou, anasemekana kuwa salama baada ya ndege ya helikopta

Thursday, December 24, 2015

MILIONI 18 TAHABANI KWA EL- NINO AFRIKA MASHARIKI



Wataalam wanasema kwamba watu wasiopungua milioni 18 katika upembe wa Afrika wameathirika na ukame unaotokana na mfumo wa hali ya hewa ya El-Nino.
Mamlaka ya Maendeleola ya Kimataifa IGAD , na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu imeonya kuwepo kwa upungufu mkubwa wa fedha ya kukabiliana na athari za El-Nino.
Watabiri wa hali ya hewa walitabiri athari kubwa kutokana na mvua ya El-Nino kwa miongo kadhaa sasa.




Monday, December 14, 2015

FURAHA YA MAASKOFU KUTOKA KWA MAKAMU WA RAIS KATIKA TAMASHA LA KRISMASI


tanzania-bishop-malasusa
Na Mwandishi Wetu
MAASKOFU wa madhehebu  mbalimbali wa Makanisa hapa Tanzania wamempongeza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kukubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo linalokwenda sambamba na Shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 kwa amani na utulivu, uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Askofu wa Kanisa la KKKT, Dk Alex Malasusa anasema ni jambo jema kumshukuru Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu kiasi cha kumpata rais mchapakazi.

Sunday, December 13, 2015

TANESCO TUMBO JOTO LEO

DAR ES SALAAM.Sospeter Muhongo,waziri wa nishati na madini

Serikali imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuacha mara moja tabia ya kukata umeme bila sababu ya msingi.
Agizo hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walipofanya ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo.
Mara tu baada ya kuapishwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walifanya ziara hiyo ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuzungumza na Menejimenti ya Shirika hilo.
Profesa Muhongo alisema wananchi wamechoshwa na tabia ya shirika hilo ya kukatakata umeme bila kuwepo na sababu ya msingi ya kufanya hivyo.
Haiwezekani kila mwaka matatizo ni yaleyale na nyie bado mpo ofisini, hili halikubaliki na