WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo
lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
la kuwataka mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe
kabla ya saa 12 leo jioni limetekelezwa.
Waziri Mkuu amepokea barua kutoka kwa Kamishna wa
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Salome Kaganda
ikithibitisha kuwa mawaziri na naibu mawaziri wote wametekeleza agizo hilo.







