Friday, March 27, 2015

AJALI TENA

Ajali ya Treni na Lori kati ya Machinga Complex na Mataa ya Chang'ombe: Wanaotumia njia hii tumieni njia nyingine

KESHO UCHAGUZI WA RAISI NIGERIA


 
Raia wa Nigeria kesho wanatarajiwa kujitokeza katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo
Hata hivyo kumekuwa na vute ni kuvute huku kuripotiwa taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayosambaza mashine za kusoma vitambulisho vya elekroniki vya wapiga kura kukamatwa na maafisa usalama wa nchi hiyo.
 Chama kinachotawala nchini humo cha PDP kimesema kwamba mtendaji huyo Musa Sani anahusishwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo cha APC ambaye anadhaniwa kutaka kuvuruga uchaguzi huo.

Chanzo: bbc

ZITO KUWASALITI WANAHARAKATI WENZAKE


Stori: Elvan Stambuli
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Zuberi Kabwe ambaye ametangaza rasmi kuwania ubunge katika majimbo mengine, amelaumiwa na waliokuwa wapigakura wake waliodai amewaacha kwenye mataa, Uwazi Mizengwe limedokezwa.
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Zuberi Kabwe.
Zitto ametangaza kwamba atagombea ubunge kwa tiketi ya chama cha ACT- Tanzania katika majimbo yafuatayo ambayo majina ya wabunge na vyama vyao yamewekwa kwenye mabano; Kahama (James Lembeli, CCM), Kawe (Halima Mdee, Chadema), Segerea (Dk. Makongoro Mahanga, CCM) na Kasulu (Moses Machali, NCCR).
Kwa mujibu wa Zitto, majimbo hayo na mengine manne ambayo hajayataja anaweza kugombea na akapata kura nyingi na kushinda na ndiyo maana alipokuwa akiliaga bunge wiki iliyopita, aliwaambia wabunge kuwa watakutana tena ukumbini humo Novemba, mwaka huu.
Novemba uchaguzi mkuu utakuwa umekwishafanyika na ni wakati ambao wabunge watatakiwa kwenda kuapishwa bungeni.Baadhi ya wapigakura wa Kigoma Kaskazini waliozungumza na gazeti hili, walisema kwamba Zitto amewaacha kwenye mataa kwa sababu kama kweli amefanya vema katika jimbo lake litakuwa ni jambo la ajabu kulihama na kwenda kuongoza kwingine.
“Ukweli ni kwamba ametushangaza. Zitto amekimbia jimbo lake la Kigoma Kaskazini kwa nini? Hajatoa sababu ya msingi, kulikoni?” alihoji Ally Said Ally aliyejitambulisha kwa simu ya kiganjani kama mpigakura wake wa Kigoma.
Mwigulu Nchemba.
“Kuna ukweli anauficha, lazima kuna sababu za msingi zinazomfanya kukimbia jimbo lake. Katika jimbo hili kuna matatizo mengi ambayo hajayatimiza ndiyo maana ametuacha kwenye mataa,” alisema mpigakura mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Mohammed.
Tamko hilo tayari limewapa kiwewe wapambe wa wabunge wa majimbo hayo na hata wabunge wanaokalia viti hivyo na kuwafanya wajiandae kupambana na Zitto ikiwa ataibukia katika majimbo yao ya uchaguzi.
“Tutapambana na ajue kwamba tutawaeleza wapigakura wetu kuwa mtu huyu hafai na ndiyo maana amefukuzwa Chadema na kukimbia jimbo lake,” alisema mbunge mmoja ambaye jimbo lake limetajwa na Zitto kwamba anaweza kugombea.
Mbunge huyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe kwa sasa kwa sababu Zitto hajasema wazi kama atakwenda katika jimbo lake alisema atasema mengi jimboni mwake ikiwa atatangaza rasmi na siyo ‘jumlajumla’ kama alivyofanya sasa.
Akizungumzia uchaguzi mkuu ujao hivi karibuni,  Zitto ambaye amejiunga na chama cha ACT alisema atagombea nafasi ya ubunge kwa kuwa umri wake haumruhusu kugombea nafasi ya urais na kwamba jimbo atakalogombea litawekwa wazi baada ya yeye kushauriana na washauri wake kwa kuwa majimbo zaidi ya sita nchini yanamtaka agombee.
“Nitasema hapo baadaye nitagombea jimbo gani kwa sababu majimbo mengi yananiita nikagombee, Kawe wanatitaka, Segerea, Kasulu, Kahama, hivyo nitazungumza na wenzangu halafu nitasema nitagombea wapi,” alisema bila kutaja sababu za kutogombea jimboni kwake Kigoma Kaskazini.
Alisema kuhamia kwake ACT ni uamuzi sahihi kwa sababu chama hicho kinaendana na kile alichokuwa anakipigania kwa miaka yote.Aliongeza kuwa amehamia ACT si kwa bahati mbaya bali anajua nini anafanya na atahakikisha chama hicho kinakua na kuvipita baadhi ya vyama vya siasa vyenye umaarufu kwa sasa.

MCHUNGAJI AZUA BALAA- KATOLIKI









Stori: Mwandishi Wetu
SIKU chache baada ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo la jijini Dar, Josephat Gwajima kumtusi Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, Polycarp Kardinali Pengo, taarifa nyuma ya pazia zimeeleza kuwa mchungaji huyo ametumwa na kikundi cha watu fulani, Uwazi Mizengwe linakupa mchapo kamili.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo la jijini Dar, Josephat Gwajima.
Gwajima alirekodiwa kwenye ibada ya kanisa lake Jumapili iliyopita ambapo ‘alimtusi’ Pengo akituhumu kuwa ni msaliti kwani amekwenda kinyume na Taasisi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kuwataka waumini waisome Katiba Inayopendekezwa kisha wapewe uhuru wa kupiga kura ya “ndiyo” au “hapana” tofauti na vyombo hivyo vyenye dhamana ya kuongoza dini ya Kikristo vilivyotaka waumini waipigie kura ya “hapana” Katiba Inayopendekezwa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Gwajima ametumwa na kikundi cha watu ambacho kinaunga mkono hoja ya kukataa Mahakama ya Kadhi kama ilivyokataliwa na vyombo hivyo vyenye dhamana ya kuongoza dini ya Kikristo hivyo kumpinga Pengo ambaye wanaamini anatetea suala la Mahakama ya Kadhi liruhusiwe.
“Gwajima anatumika tu anamkashifu Pengo ili kumchafua na asiweze kusimamia hoja yake ya kuwaacha wapigakura waamue wenyewe kuikubali au kuikataa Katiba Inayopendekezwa wakiamini watu wanaweza kuipigia kura ya “ndiyo” na suala hilo likajadiliwa wakati wenzake wamelipinga,” kilisema chanzo hicho.
Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, Gwajima ametumika kumchafua Pengo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuhofia huenda akawa na upande wa mgombea ambaye anampigia chapuo ili apitishwe.
“Siyo tu kuhofia Mahakama ya Kadhi, Gwajima ametumika kumchafua Pengo kwa hofu kuwa huwenda akawa ana mgombea wake anayemtaka awe rais,” kilisema chanzo hicho.
Jitihada za kumpata Gwajima ili aweze kuzungumzia madai hayo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani lakini gazeti hili liliweza kuzungumza na mmoja wa viongozi wa chini yake aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini ambapo alisema Gwajima anatumika na Roho Mtakatifu na si vinginevyo.
“Mchungaji (Gwajima) ametumwa na Roho Mtakatifu kusema yale aliyoyasema hakutumwa na mtu wala kikundi chochote cha wanasiasa,” alisema kiongozi huyo.

LOWASA Vs MEMBE BALAAA


Na Erick Evarist
Zikiwa zimebaki siku  218 kufikia Oktoba 20, siku ya uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mgombea wa urais kupitia chama hicho bado ni kitendawili.
Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Ngoyai Lowassa.
Kitendo cha CCM kuchelewesha kupiga kipyenga cha kuanza kwa mbio hizo, kimepandisha homa kali ya uchaguzi miongoni wa Watanania, huku kambi za waonesha nia mbalimbali zikiendelea kuundwa na kuimarishwa, wapambe wakihama kutoka kambi moja kwenda nyingine.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa pamoja na waonesha nia kuwa wengi, kambi zenye nguvu ndani ya chama cha mapinduzi zinazooneshana ubabe kila siku ni  za makada wawili wakongwe wa chama hicho, Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Ngoyai Lowassa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Taarifa  za uhakika kutoka ndani ya chama hicho zinadai kuwa kambi za wawili hao  kadri siku zinavyozidi kusonga zimekuwa katika mapambano  makali na zikibuni kila aina ya mbinu ili kuhakikisha zinajiimarisha na kutunisha misuli itakayoweza   kuwashawishi wajumbe wa Kamati Kuu (CC), Halmashauri Kuu (NEC) na Mkutano Mkuu kupitisha jina lake.
Kada Lowassa ambaye jina lake linatamkwa sana midomoni mwa watu anapigana kwa staili ya  ‘juu ya ardhi’  huku  usiku na mchana  akijenga hali kukubalika na wananchi  kuliko wagombea wenzake ili kupata nguvu kubwa ya kukitishia chama chake kisithubutu kulikata  jina lake,  iwapo kuna vigogo ndani ya chama   chake wana mpango wa kufanya hivyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Mtindo huu wa Lowassa umemfanya aonekane ndiye mwenye mvuto zaidi kwa wananchi kuliko wagombea wenzake, hasa pale vinapojitokeza vikundi vya watu mbalimbali wakimshawishi achukie fomu kugombea urais, wakati yeye mwenyewe hajatangaza nia.
Wakati Lowassa akitumia mtindo wa juu ya ardhi, Kada Membe anadaiwa kutumia mtindo wa nyambizi wa kwenda chini ya maji bila kuonekana, kambi yake ikifanya kazi kimya kimya usiku na mchana ili itakapoibuka mbele ya safari iishangaze kambi ya Lowassa kwa jinsi atakavyokuwa na nguvu, ingawa kwa mtindo wake wa kupambana hivi sasa watu wengi wanaona kama hana mvuto.
Mtindo mwingine  wa kupambana unaotumiwa na kambi hizi ni wakupandikiziana ‘wapelelezi’, wapo watu wanaomuunga mkono Membe lakini hutumika kutoa taarifa kwenye kambi ya Lowassa na wapo walio katika kambi ya Lowassa ambao hutoa taarifa kwa kambi ya Membe.
Chanzo kingine ndani ya chama hicho kimekazia kuwa kuna baadhi ya wagombea wa urais wanaotajwatajwa, wamejitokeza lakini kila mmoja ana mgombea wake (kati ya Lowassa au Membe) ili pindi jina la mmoja kati ya wawili hao litakapopitishwa, waunganishe nguvu kwa mgombea huyo kwa ahadi za kupewa madaraka.
“Kuna baadhi ya wagombea wanafuata tu mkumbo ili atakapopita mtu wake, anawachukua watu wake na kuwaunganisha kwa mtu huyo aliyepita,” kilisema chanzo hicho.Hata hivyo mitindo hii ya  ‘juu ya ardhi’ na ‘nyambizi’ inayotumiwa   na kambi za makada hawa  wawili, wenye nafasi kubwa ya kupitishwa na chama chao kugombea urais, inafanya iwe ni kazi ngumu sana kujua ni nani mbabe kati yao.
Wachambuzi wa mambo ya siasa wanadai kitakachothibitisha nani ni mbabe ni kipyenga cha mwisho baada ya vikao vya juu vya maamuzi ya Chama Cha Mapinduzi kupitisha jina moja.

DONDOO ZA MAGAZETI YA LEO

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC_0538
.
DSC_0539
.
DSC_0540
.
DSC_0541
.
DSC_0542
.
DSC_0543
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC_0557
.
.
.
.
.
.
.
.
.