Mafuriko mabaya kazkazini magharibi mwa Tanzania yamewaua takriban watu 38.
Maafisa
wa polisi wanasema kuwa mvua kubwa na upepo mkali ziliharibu nyumba na
kufunga barabara karibu na mji wa Shinyanga na hivyobasi kuzuia
oparesheni za kuwanusuru watu.Wanasema kuwa mamia ya watu wamewachwa bila makao huku zaidi ya watu 60 wakijeruhiwa.
Waandishi wanasema kuwa mimea imeharibiwa na mifugo kuuawa.
No comments:
Post a Comment